Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Nendeni mkawapokee zenu Mamelodi

Mamelodi Sundown 68.heic Mamelodi Sundowns.

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa hawana vita ya nje ya uwanja na Mamelodi Sundowns lakini vita yao itakuwa uwanjani dakika ya dakika 90 za mchezo wao.

Kamwe amesema hayo wakati wa hamasa kuelekea mchezo wao dhidi ya Masandawana utakaopigwa Jumamosi, Machi 30, 2024 katika dimba la Mkapa.

"Sisi hatuna vita na Mamelodi Sundowns, hatuwachukii, kama wapo wengi waje kwa wingi uwanjani. Young Africans SC lugha yetu ni amani, hatupigi wala kuzuia mtu kuja kwa Mkapa.

"Kama mnataka kwenda kuwapokea ndugu zenu nendeni wanafika Alhamisi. Ugomvi wetu na Mamelodi utakuwa kwenye Dakika 90 Uwanjani. Wote mnakaribishwa kwa Mkapa.

"Tunafurahi kuona wachambuzi na Makolo wanawasifu wachezaji wa Mamelodi ili tukiwafunga wakose cha kusema, tuwe tumezipiga timu tatu. Hakuna raha kama kuzifunga timu tatu kwa pamoja. Mamelodi, Makolo na Wachambuzi," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: