Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Mashabiki msijiaminishe tutawafunga Simba bao nyingi

Kamwee WA0025 Kamwe: Mashabiki msijiaminishe tutawafunga Simba bao nyingi

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wao kama Yanga wanaichukulia Simba SC kama timu tishio kwenye Ligi ya Tanzania na timu za Afrika Mashariki na Kati kutokana na ubora wao.

Kamwe amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kuelezea Mipango ya Timu yake kuelekea katika Mchezo wa Derby ya Kariakoo Dhidi ya Simba SC Mchezo ambao utachezwa Aprili 20 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

“Hizo hadithi ambazo mpo nazo kwenye mitandao ya kijamii na magrupu ya WhatsApp kwamba tunakwenda kumpiga mtu bao 20, au bao nyingi, ninaomba mzibadilishe, focus yetu iwe kwenda kutafuta alama tatu. Mwisho wa msimu hatutakuwa mabingwa kumpiga Simba bao 100, bali kwa kuwa na alama nyingi kuliko timu inayoshika nafasi ya 2.

“Alama tatu ndizo za muhimu zaidi, tukishinda bao 1-0, au 2-1 au 3-2, alama tatu ndiyo muhimu zaidi. Mabao haya yatakuja tu kutegemea nay eye amemaka vipi, wakijichanganya watakula nyingi. Hata Novemba 5, mabao matano yalikuja tu lakini sisi ajenda yetu ilikuwa alama tatu, Simba akajichanganya akala mkono.

“Najua Wanayanga mnajiamini, mnaiamini timu yenu, twendeni kwa wingi kwa Mkapa, wachezaji wanwahitaji mno. Wiki hii tusiwafuate wachezaji mitandaoni, tuwaache wajiandae kutupa ushindi siku ya Jumamosi," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: