Yanga imeendelea kutoa dozi ya tano tano katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa JKT Tanzania 5-0 katika mechi iliyopigwa Jumanne hii usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa kikosi chao kiko imara na malengo yao msimu huu ni kuchukua mataji yote ya ndani na kufanya vizuri kimataifa.
"Ndani ya Siku 9 [kutoka Agosti 20 mpaka jana, Agosti 29]. Young Africans Sports Club Tumecheza mechi 4.
"Mechi Mbili za Caf Champions League [ Vs Asas kutoka Djibouti] na mechi mbili za Ligi Kuu ya NBC [ Vs KMC & JKT Tanzania].
"Kwenye hizo mechi 4, Yanga, Tumefunga Magoli 17 na Tumeruhusu Goli 1 tu langoni mwetu. Cha kuvutia zaidi, kwenye haya magoli 17, Magoli 2 yamefungwa na Mabeki. Magoli 5 yamefungwa na Washambuliaji na Magoli 10 yaliobaki yamefungwa na viungo.
"Jumla ya wachezaji 9 kwenye kikosi chetu wamehusika kwenye kufunga magoli 17 tuliyofunga kwenye mechi 4.
"Kubwa kuliko ni hii sasa, Jumla ya wachezaji 25 kati ya 28 waliosajiliwa kwenye kikosi cha Yanga msimu huu Wameshapata dakika za kucheza uwanjani.
"Ni golikipa Mshery, Skudu [Aliyekuwa majeruhi] na Kinda Shaibu tuliyempandisha kutoka kikosi cha vijana cha U 20 ndio hawajacheza. Hii ndio Yanga ya Gamondi Mabibi na Mabwana," ameandika Ally Kamwe.