Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Hatutatoa 'Thank You' tena

Kamwe Ms Yanga Kamwe: Hatutatoa 'Thank You' tena

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imesema kuwa imebadilisha utaratibu wa kuwaaga wachezaji wake baada ya kubaini kuwa mtindo wa kuwapost kwenye mitandao ya kijamii unawashushia thamani wachezaji hao.

“Kuhusu Thank You za wachezaji hapa tunataka tuwafundishe na timu nyingine. Kumuaga mchezaji kuna madhara ya aina mbili, kwanza mmeishi na mchezaji kwa miaka kadhaa, mkimpa Thank You mashabiki wanaweka kichwani kwamba hafai.

“Kama watu wanafikra hasi juu ya hilo kwa nini mnaendelea nalo na kumpa wakati mgumu huyu mchezaji kwenye maisha yake ya soka. Unakaa siku nzima kuandaa habari ya kumpa Thank You mchezaji halafu comment zake kwenye kurasa zinakuja negative kila shabiki anamponda, inaleta picha mbaya hata kwa timu anayokwenda hata kama mmeachana na mchezaji kwa Amani tu.

“Jambo hilo tumeona halina manufaa kwetu japo taarifa ni muhimu umma unatakiwa ujue kuhusu mchezaji flani iwapo tuko naye au la! Lakini lisiwe jambo la kutengeneza hype. Kwa sasa tumekuja na utaratibu mpya wa kuaga wachezaji wetu kupitia huduma mpya ambayo tumaianzisha ya Yanga Habari, ukijiunga utapata taarifa zote kwa utaratibu mzuri.

"Leo tumezindua mfumo mpya wa kupata habari ujulikano kama "Yanga Habari" haijalishi una simu ya namna gani lakini unaweza kupewa taarifa na Klabu ya Yanga SC. Ukijiunga na mfumo huu utapata ujumbe kutoka Klabu ya Yanga ikikupa taarifa mbalimbali,” amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live