Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Blichi nilienda nalo kuzimu, nakwenda nalo Misri

Kamwe Hospital 0004 Kamwe: Blichi nilienda nalo kuzimu, nakwenda nalo Misri

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni February 27, 2024 ambapo Ofisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amekutana na Vyombo vya Habari na kuzungumza haya.

“Pacome Day ndio lilikuwa tukio kubwa la kimichezo barani Afrika kila Mtu alihamasika, Rais wa Nchi Dkt Samia Suluhusu alisema Yanga SC imefurahisha Nchi hivyo ni wajibu wetu kuendelea kufurahisha Nchi”

“Kuelekea mchezo wa CR Belouizdad huwezi kuacha kutambua mchango mkubwa wa Mashabiki ambao walihusika kuanzia maandalizi ya Hamasa ya Pacome Day, Nchi nzima ilimeremeta bleach ikiwa lengo la kumuunga mkono na kuheshimisha mchezo”.

“Hili blichi nilizimia nalo na kuzinduka nalo na kwa heshima ya Pacome nitakwenda nalo Mısri hivyo Wananchi msiwe na haraka ya kufuta bleach endeleeni kushangilia, Waarabu wajiandae kama wamejiandaa kumkaba Pacome, watakutana na Pacome wengi sana kwa sababu bado Wachezaji wetu wanalo,” Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live