Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Aziz KI alituepusha na aibu nzito kwa Mkapa

Aziz Ki Goli Bora Kiungo wa Yanga, Stephane Aziz KI

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema huwa akimwangalia kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Stephanie Aziz KI huwa anajikuta anamshukuru kwa jinsi alivyowaokoa na aibu mbele ya Simba.

Kamwe amesimulia hayo kwenye makala maalum ya Yanga ikielezea mambo ya msimu uliopita walioweka rekodi kubwa ya mafanikio.

Kamwe amesema bao ambalo Aziz KI aliwafunga Simba akiisawazishia timu yao kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi baina ya timu hizo lilikuja wakati muafaka.

"Unajua tumetoka kupoteza dhidi ya Al Hilal na tumetolewa tunarudi nyumbani tunakutana na Simba na hapo watani wetu wametoka kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mtaona hali ilivyo," amesema Kamwe

"Mechi na Simba inaanza wanapata bao ilikuwa ni ngumu sana kukubalika lakini Aziz KI akafanya kweli bonge la bao akafunga, huwa nikimuangalia nasema kama Kuna eneo alitufaa basi ilikuwa pale."

"Alithibitisha kwamba mchezaji mkubwa anaonekana kwenye matokeo makubwa lilikuwa bao muhimu sana kwa Yanga."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: