Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Azam Complex iitwe Yanga Complex kuanzia sasa

Ali Kamwe Masimango Ally Kamwe.

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amewatupia dongo Klabu ya Azam baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Klabu ya Bahri ya nchini Ethiopia jana usiku kwa mikwaju ya penati.

Kamwe amedai kuwa kwa vile Uwanja wa Azam Complex unatumiwa na Yanga, basi ubadilishwe jina na kuitwa Yanga Complex Chamazi mpaka pale ambapo Yanga italerejea kutumia dimba la Mkapa ambalo linakarabitwa.

"Tunatuma maombi kwa TFF na Bodi ya Ligi ule uwanja ubadilishwe kuanzia sasa uitwe Yanga Complex. Tunakwenda kimataifa, tukiulizwa na CAF, Yanga ni timu, je, hii Azam ni nini? Tutajibu nini? Ni kiwanda au nini? Kwa hiyo tutaita Yanga Complex mpaka tutakapoondoka pale.

"Azam hakuna timu pale, kesho (leo) tukutane Yanga Complex Chamazi, anayebisha alete timu pale. Kesho (leo) tunakwenda kutambulisha Maxi Day pale na kuutambulisha rasmi ule kuwa uwanja wetu," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: