Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwaga afunguka kung'atuka Simba SC

E7ebSKiXIAQ7W3n Afisa Habari wa Simba Sc, Ezekiel kamwaga

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya taarifa kusambaa kwa kasi kuwa Kaimu Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga amebwaga manyanga ndani ya kikosi hicho.

Kamwaga alichukua mikoba ya aliyekuwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ambaye alichimba kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na uongozi.

Alipotafutwa Kaimu Ofisa Habari wa timu hiyo Kamwaga kwa njia ya simu hakuweza kupokea hivyo jitihada bado zinaendelea.

Lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kamwaga ameandika;

"Nimeshangazwa na taarifa hizi zinazosambazwa na waandishi wenzangu - wengine wazoefu, kuhusu mimi kubwaga manyanga Simba Wengine wamenipigia simu ku 'balance' wakati tayari wameshasababisha taharuki isiyo na sababu kwa viongozi wangu, wanachama wenzangu na washabiki wa Simba kwa ujumla".

"Nimepewa majukumu yangu mahususi Simba kwa muda wa miezi miwili na bado kazi hiyo sijaikamilisha. Nimedhamiria kukamilisha majukumu hayo mpaka ukomo wake Baada ya kuona usajili wa aina yake na mipango mikubwa mikubwa ya Simba ikiwa inatekelezwa, wabaya wetu wameibuka na uongo mwingine. Njia ya mwongo ni fupi".

Mimi bado nipo Simba. Tena bado nipo sana. Uongo huu dhidi yangu na Simba SC upuuzwe",ameandika Kamwaga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live