Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamungo bado hajaitema Stars

Kamungo Messiii.png Bernard Kamungo na Lionel Messi

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji kinda wa Kitanzania, Bernard Kamungo baada ya kuzuka kwa taharuki kwa mashabiki na wapenzi wa soka la Tanzania kufuatia kuitwa kwake Timu ya Taifa la Marekani kwa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya 2024.

Kamungo amesema hayo wakati akijiandaa kuripoti kambini kwani anaamini hiyo ni fursa ya kukua zaidi kama mchezaji kwani kucheza kwake ngazi ya vijana hakumzuii kuichezea Timu ya Taifa ya Tanzania wakati akihitajika.

“Ni moja ya ndoto yangu,” alisema Kamungo. “Ni ndoto pia ya familia yangu kuitwa kwenye Timu ya Taifa ya Marekani na kuweza kuhudhuria kambi. Hii ni fursa na ni muhimu kuichukulia kwa mtazamo chanya, bado haijafika hatua ya kusema ndio basi tena Tanzania, Olimpiki ni kwa ajili ya vijana.”

Kamungo aliwahi kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars mwezi Juni lakini hakutumika licha ya kocha wa kikosi hicho, Adel Amrouche kuwa na mipango naye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live