Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Yanga haitaimiliki Yanga, bali Yanga itamiliki kampuni - Hersi

Arafat Haji X Hersi Oktoba 25 Eng. Hersi.

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi said amesema kuwa wameweka muundo bora wa uongozi ili kuhakikisha wawekezaji wanaokuja kuwekeza kwenye klabu hiyo wanapata manufaa wanayoyataka badala kufanyiwa ujanja ujanja.

Hersi amesema hayo wakati akizungumzia kuhusu mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji ambayo wanaendelea kuyafanya ndani ya klabu tangu aingie madarakani.

"Tunajenga mfumo ambao mwekezaji akija anakuta muundo bora wa utawala, kimapato. Malengo yetu ni kuhakikisha kuwa na timu imara kiuchumi ili yule anayekuja awe na uhakika wa kile anachowekeza kwenye timu.

"Hivyo tumezingatia sana usalama wa biashara kwa kila ambaye ana nia ya kuwekeza kwenye Klabu yetu.

"Ili kulinda maslahi ya wawekezaji tumehakikisha kuwa lazima tuwe na Makubaliano ya kimkataba. Vile vile tumelinda maslahi ya Klabu kwa kuhakikisha kuwa kinachopelekwa kwenye kampuni ni nembo na biashara ya timu.

"Mali zote za Yanga zinabaki kuwa mali ya Yanga na sio mali ya kampuni. Kampuni mpya ya Yanga haitaimiliki Yanga, bali Yanga ndio itamiliki kampuni. Mwekezaji hana haki na mali za klabu kama vile uwanja na majengo," amesema Eng. Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live