Mdau wa soka, Stanley Kambona amesema michuano ya Afcon 2027 ichukuliwe kama sehemu ya nchi na wadau wa teknolojia kuinuka huku akiishauri Serikali kuwaita Zaidi wadau ikiwemo makampuni ya simu.
“Tunaitazama michuano hii kama sehemu ya nchi na wadau wa teknolojia kuinuka katika kuwekeza zaidi kwenye upande wa teknolojia, Serikali kuna namna inaweza ikawa inakwamisha wadau ambao wanatamani sana kuwekeza kwa upande wa teknolojia kutokana na sera zilizopo na baadhi ya watu.
Kuweka vikwazo kwa maslahi yao binafsi lakini ni kitu ambacho kinapelekea nchi kurudi nyuma, mfano tukiangalia kwa sasa tuna makampuni manne ya simu lakini nchi kama Tanzania isingepaswa kuwa na makampuni manne ilipaswa kuwa na makampuni zaidi ya manne.”
Kambona amesema hayo leo Jumatano Oktoba 4, 2023 wakati wa mjadala wa Mwananchi Space ulioandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd ukiwa na mada isemayo; Fursa zilizopo kwa Tanzania kuandaa fainali za Afcon 2027.