Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kambi ya Simba gharama kwelikweli

Wachezaji Wa Simba Kambi ya Simba gharama kwelikweli

Sat, 14 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MSAFARA wa watu 20 wa Simba upo Morocco katika Mji wa Rabat kwenye moja ya hoteli ya kifahari kwenye eneo hilo.

Mwanaspoti linajua Simba imejichimbia katika hoteli ya Dawliz Resort & Spa, ambayo kwa siku moja chumba cha watu wawili unatakiwa kulipa si chini ya Sh390,000.

Katika msafara huo kuna vyumba vitano ambavyo vitatumiwa na watu wa benchi la ufundi kila mmoja kulala cha kwake ambacho thamani yake si chini ya Sh400,000.

Kwa maana hiyo Simba kwa siku moja vyumba 15, ambavyo watalala watu wawili watakuwa wanalipia si chini ya Sh5.8 milioni kwa ajili ya kulala pamoja na kupata kifungua kinywa.

Vyumba vitano ambavyo watatumia benchi la ufundi kwa siku 15, watakazokuwa hapo Rabat watakuwa wanalipa si chini ya Sh6 milioni.

Kwahiyo idadi ya watu ishirini waliokuwepo katika msafara wa kwanza ndani ya siku 15 watakazokuwa nchini humo kulala na kunywa chai watalipia si chini ya Sh11.8 milioni.

Simba watalazimika kuingia gharama nyingine kama kunununua chakula na vinywaji kwa ajili ya mchana na usiku ndio maana wamesafiri na mpishi wao, Samuel Cyprian ambaye anawajulia vilivyo.

Wakati huo huo msafara huo utaingia gharama nyingine ya kulipia usafiri wa ndani, uwanja wa mazoezi na mambo mengine ya msingi.

Pesa hiyo inaweza kuzidi kwani jana Agosti 12, msafara wa Simba awamu ya pili wa wachezaji pamoja na viongozi uliondoka Tanzania kuelekea Rabat kuungana na wenzao.

Ukilipa pesa hiyo unapata chai asubuhi bure ila chakula cha mchana na usiku msafara huo wa Simba unatakiwa kujitegemea wenyewe.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz