Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kambi ya Kiduku yamjibu Mcongo kuhusu ubora wa Mwakinyo

FOzrGwQXEAAbp7P Bondia Twaha Kiduku akitupa Konde kwa Bondia Mkongo, Alex Kabangu

Sun, 27 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Saa chache baada ya Alex Kabangu kumtaja Hassan Mwakinyo kuwa ndiye bondia bora nchini Tanzania, kambi ya bondia Twaha Kiduku imemjibu  bondia huyo wa DR Congo ambaye siku wa kumkia leo amechapwa kwa pointi na Kiduku.

Kabangu muda mfupi baada ya kuchapwa na Kiduku kwa pointi mjini Morogoro, alimtaja Mwakinyo kuwa ndiye bondia bora kati ya mabondia wa Tanzania.

"Kwa Tanzania, Mwakinyo ndiye bondia bora, hakuna zaidi yake," alisema Kabangu, kauli ambayo kocha wa Kiduku, Power Iranda amesema ni ya mkosaji.

"Yeye akubali akatae amepigwa bila ubishi, hayo ya kumtaja Mwakinyo kuwa ndiye bondia bora ni maneno ya mkosaji tu," amesema kocha huyo wa muda mrefu wa Kiduku.

Amesema Kabangu kumtaja Mwakinyo kuwa ni bora baada ya kupigwa na Kiduku ni kama anataka kutengeneza njia ya kucheza pambano na bondia huyo.

"Anataka tu kuwa kwenye midomo ya mashabiki wa ngumi, kusema Mwakinyo ndiye bondia bora kwenye pambano la Kiduku ni kutengeneza tu sintofahamu kwa mashabiki, ingawa binafsi namuona Kiduku ni bora zaidi.

Amesema Kabangu ni kama amekutana na sapraizi ambayo hakuitarajia kutoka kwa Kiduku, na hakutegemea Kiduku angebadilika na kucheza ngumi licha ya kutaka kumtoa kwenye mchezo lakini imekuwa tofauti.

"Baada ya kuona mbinu zake ikiwamo kucheza faulo kushindwa kufanikiwa, ameamua kumtumia Mwakinyo, hayo ni maneno ya mkosaji, akubali amepigwa ili akajipange upya," amesema.

Mmoja wa viongozi wa Kabangu, Robert Kalisa amesema Kiduku ni bondia mzuri na amecheza vizuri na wanajipanga kwa mchezo wa marudiano baadae Julai.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz