Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya saa 72 kuamua nini kifanyike Simba, Yanga kuahirishwa

Tplb Pic Data Kamati ya saa 72 kuamua nini kifanyike Simba, Yanga kuahirishwa

Mon, 10 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BAADA ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga kuahirishwa juzi Mei 8, 2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa bila kutoa sababu hatimaye Bodi ya Ligi imetoa maelezo.

Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo, imeeleza kuwa kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu mchezo huo ulipangwa kuanza saa 11:00 tarehe nane katika uwanja wa Mkapa lakini saa saba mchana ratiba hiyo ilisogezwa mbele hadi saa 1:00 usiku.

 Bodi ya Ligi meeleza kuwa mabadiliko hsyo iliyapokea kutoka kwenye Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ maelekezo ambayo yalizingatiwa na kutekelezwa kwa mujibu wa kanuni za bodi hiyo ya kutii maelezo ya FIFA, CAF na TFF.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kupitia Bodi ya Ligi timu husika zilipewa taarifa rasmi ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo pia mashabiki waliokuwa uwanjani walitangaziwa huku pia wakiweka machapisho ya tangazo hilo kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za bodi hiyo na TFF.

Baada ya Bodi ya Ligi kujiridhisha kuwa timu zote zimepata taarifa, taratibu za mchezo kuanza saa 1:00 usiku ziliendelea ikiwemo uhakika wa miundombinu, usalama na taratibu za mashabiki kuingia uwanjana.

Bodi imeendelea kufafanua kuwa, timu ya Yanga iliwasili uwanjani hapo saa 10:20 na kuingia eneo la kuchezea saa 10:35 jioni kwaajili ya kupasha moto midulo hadi saa 10:50 jioni walipomaliza na kurejea vyumbani. Wachezaji na benchi la ufundi waliingia tena uwanjani saa 11:10  na kukaa kwa dakika 10 kabla ya kurejea vyumbani.

Hata hivyo Mwanaspoti lililokuwa uwanjani hapo lilishuhudia Yanga wakiingia kwa mara ya pili uwanjani (Pitch) saa 10:58 wakiwa wmaevalia jezi zao za mechi na kuondoka saa 11:17 muda ambao ni tofauti na ilioainisha bodi ya ligi. Taarifa ya Bodi inaeleza kuwa wachezaji na viongozi wa Yanga waliingia kwenye gari la timu hiyo na kuondoka uwanjani hapo saa 11:40 jioni.

Kabla ya hapo klabu ya Yanga ilitoa taarifa kuwa wamesikitishwa na mabilidiliko hayo ya muda ambayo ni kinyume cha kanuni ya Ligi kuu 15 (10) ambayo inahusu taratibu za mabadiliko ya mchezo ibayoeleza kuwa mabadiliko yanapaswa kufanyika kabla ya masaa 24 ya muda wa mchezo kuanza.

Yanga katika taarifa yao walieleza kupinga mabadiliko hayo na kupeleka timu uwanjani kwa muda uliopangwa awali na kuitaka Bidi ya Ligi kuzingatia kanuni katika maamuzi yake.

Simba waliwasili saa 11:25 jioni na kuendelea kuwepo katika eneo hilo hadi pale walipopata taarifa ya kahirishwa kwa mchezo huo.

Timu zote mbili hazikukaguliwa na waamuzi kama ishara ya kuanza rasmi kwa taratibu za mchezo huo.

Taarifa inaeleza kuwa baada ya kujiridhisha kuwa Timu ya Yanga imeondoka uwanjani pale kukiwa hakujafanyika taratibu zozote za kuanza mchezo, Bodi ya Ligi baada ya Mashauriano na mamlaka nyingine za usalama na ulinzi na kwa mazingatio ya kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom (kanuni 10(1) na 10(2)), ilituma kwa kirabu shiriki taarifa rasmi za kuahirishwa kwa mchezo huo.

Sambamba na hilo simba haikutoa taarifa yoyote kabla ya saa 11:00 wala saa 1:00 na baada ya mechi kuabyirishwa, siku moja mbele walitoa kauli ya klabu ambayo inaeleza kuwa wao walipokea taarifa ya kubadili muda na kuitii huku wakiishutumu Yanga kwa kutotii taarifa hiyo.

Sekretariati ya Bodi ya Ligi tayari imepokea taarifa zote kuhusiana na mchezo huo kutoka kwa maofisa mbalimbali waliopewa jukumu la kusimamia wakiwemo kamisaa na mwamuzi.

Bodi imeendelea kueleza kuwa kwa mazingatio ya kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom (kanuni 10(2) na 10 (4) usimamizi wa ligi) kikao cha kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi maarufu kamati ya saa 72 kitakutana leo Mei 10, 2021 kuweza kujadili mchezo huo kati ya Simba na Yanga uliokuwa uchezwe Mei 8.

Taarifa hiyo ni kutoka katika idara ya habari na mahusiano ya Bodi ya Ligi  Kuu Tanzania.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz