Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya Hamasa Timu za Taifa yakusanya Milioni 800

Taifa Stars AFCON Vazi Kamati ya Hamasa Timu za Taifa yakusanya Milioni 800

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Hivi karibuni Kamati ya Hamasa inayohamasisha timu za Taifa ilifanya harambee kuzichangia timu hizo ambapo ahadi zilizotolewa zilifika Sh4 bilioni na hadi leo Alhamisi fedha zilizoingia ni Sh800 milioni.

Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam ikiongozwa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa ambaye ameitaka kamati hiyo ifanye mambo matatu, kuandaa taarifa ya ahadi mpya na zilizokusanya na kumpelekea kila baada ya wiki mbili.

Pia kamati imetakiwa kufika Dodoma mwishoni mwa mwezi huu Januari na kumpa taarifa ya makusanyo na imetakiwa kufanya promosheni ya nguvu na hamasa kubwa kuzichangia timu hizo ikiwemo kuwafukia zaidi wadau wapya kuchangia.

Akizungumza leo Alhamis, Mjumbe wa kamati ya hamasa, Patrick Kahemela alisema kuwa wadau wote waliotoa ahadi hizo wanapaswa kulipa huku akiwaomba wadau wapya kuendelea kuzichangia timu hizo.

Chanzo: Mwanaspoti