Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kama tulishangaa ndevu za Morison sasa ni drama za Chama

Chama Morrison Kama tulishangaa ndevu za Morison sasa ni drama za Chama

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pale Simba aliwahi kupita Emmanuel Okwi na bado aliondoka, Nyanda bora kuanzia miaka ya 2000 Juma Kaseja naye aliondoka Daima Simba ni timu kubwa hapa Tanzania nafikiri wangeachana na hizi Drama za Chama.

Ukubwa wa Club unakuja pia kwa kukubali nyota wako kuondoka Mzee Ferguson alimuachia David Beckham katika ubora wake ni juzi tu Manchester City walikubali kuachana na Ilkey Gundogan hauwezi kuwa timu kubwa ikiwa unaogopa kufanya maamuzi magumu.

Sijui kwanini wanaendelea kumng'ang'ania au labda hofu Yanga wanamtaka lakini kuendelea kufanya hivi ni kujitukana wenyewe hata Roben Van Persie aliondoka Arsenal kwenda United, Arsenal wakiwa bado wanamuhitaji lakini kwa heshima ya Club babu Wenger alimuachia Captain kuondoka.

Karibuni hapa Chama amekuwa hana maajabu kwenye Uzi wa Simba muendelezo wake sio kama ule wa misimu kadhaa kabla ya kwenda Barkane amekuwa na panda shuka nyingi sana na Drama kibao.

Marekani wanamsemo wao maarufu for God and For the People, nafikiri For Club and For the Fans wangemalizana na Chama bila hofu anakwenda wapi hii ingesaidia sana viongozi ku focus na mambo mengine makubwa kwa msimu unaokuja.

Hata Yanga walikubali kumuachia Bernard Morison kwenda Simba vipi kuhusu Ibrahim Ajib lakini maisha yaliendelea vizuri soka lipo hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live