Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kama si Shikhalo, Aucho angetua Msimbazi

Shikhalo Pic Data Golikipa wa Yanga, Faroukh Shikhalo

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Golikipa wa Yanga Mkenya Farouk Shikhalo ndio sababu kubwa hasa ya Timu ya Yanga kutamba hii leo, juu ya kumsajili Kiungo wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho la sivyo angesaini kwa watani wao Simba SC.

Kiungo huyo kabla ya kufanya maamuzi yoyote aliwasiliana na kipa huyo kisha akataka kujua kama Yanga inalipa wachezaji kwa wakati akiambiwa kwamba timu hiyo hailipi vizuri.

Hata hivyo majibu ya Shikhalo yalimaliza kila kitu akimwambia mpaka wanamaliza mechi ya mwisho hakukuwa na madai yao yoyote na kwamba hawajawahi kucheleweshewa malipo.

Majibu hayo yalimsukuma kiungo huyo kujaa katika 18 za mabosi wa Yanga akiwaambia kwamba anakuja baada ya kujiridhisha.

Chanzo: Mwanaspoti