Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kama masihara Madrid yaongoza Laliga

F65458fc45db81ec26403739186fb802 Nyota wa Real Madrid

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Licha ya mwendo wao wa kusuasua, klabu ya Real Madrid sasa imekaa kileleni mwa msimamo wa Laliga mara baada ya ushindi wao wa mabao 2-1 walioupata jana katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Elche.

Mabao ya Vinicius Junior na Mariano yametosha kuwavusha Madrid hadi nafasi ya kwanza ambapo wanalingana pointi dhidi ya Sevilla na Real Sociedad tofauti ikiwa ni mabao ya kufunga na kufungwa.

Madrid waliingia katika mchezo huo bila ya mshambuliaji wao Karim Benzema ambaye ni majeruhi hata hivyo kazi nzuri ilifanywa na Vinicious la Modrid ambao walionekana kuwa moto kwa wapinzani wao.

Kwa upande wa Elche nyota wao Raul Gutti alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea faulo Toni Kroos. Bao la kufutia machozi ka Elche lilifungwa na Pere Milla.

Chanzo: www.habarileo.co.tz