Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kama hutaki presha usiende Simba na Yanga - Ambangile

Ambangile Yanga Kama hutaki presha usiende Simba na Yanga - Ambangile

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka George Ambangile kupitia Wasafi FM, amesema kama Kocha hataki kufundisha kwa presha (msukumo) anatakiwa asiende timu kubwa kama Simba SC au Yanga SC kwa sasabu vilabu hivyo vina mashabiki wengi wenye mitazamo tofauti.

Ambangile amesema hayo kufuatia Klabu Simba kumfukuza kocha wao, Robertinho baada ya kipigo cha bao 5-1, kutoka kwa watani zao Yanga SC.

"Binafsi sidhani kama inawezekana kufanya kazi Simba au Yanga bila presha ya mashabiki. Yani kama hutaki kupata presha kwa mashabiki basi kafanye kazi kwenye klabu tofauti na hizi klabu mbili.

"Na sio kwa Tanzania tu, kwa nchi yeyote ukienda kisha ukaambiwa hii ni klabu kubwa hapa nchini basi tegemea presha kubwa kutoka kwa mashabiki, yani ikishakuwa klabu kubwa basi ni klabu yenye mashabiki, mashabiki wenye mitazamo tofauti. Kama hautaki presha kubwa basi tafuta klabu ndogo, huko utafanya kazi miguu ikiwa juu.

"Na hiki ndicho kipindi hawa viongozi tunajua kwa kiasi gani wana utimamu wa akili, kuendana na presha ya mashabiki kipindi hiki ndicho kipindi cha kujua ubora na utimamu wa kiongozi.

"Kiukweli sio kipindi rahisi na sitamani hata kuvivaa viatu vya viongozi wa Simba sababu ni kipindi kigumu mno," amesema George Ambangile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: