Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kama huna ushahidi ka kimya-Jemedari Said

SAID JEMEDARI 1140x640 Jemedar Said

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuzuka kwa tabia ya watu kuzusha maneno ya rushwa pindi timu za Simba na Yanga zinapopata matokeo mbele ya timu zingine za Ligi Kuu Tanzania Bara.

mchambuzi mahiri wa masuala ya Soka Jemedari said ameibuka na kukemea suala hilo huku akusisitiza ubora wa vikosi hivyo , walimu wenye uwezo ndio hasa siri ya kufanya vyema katika michezo yao.

"imeanza kuudhi Simba wakishinda na Yanga wakishinda. Linatokea kundi la watu unaowaamini na wanasema kuwa ushindi huo una makandokando ya Rushwa. Umefika muda wa wadau kutoa ushirikiano kwa Vyombo vya Uchunguzi. Watu ni kama vile hawaamini tena kama timu zetu zinaweza kushinda kwa kushindana kiwanjani. Wanaoamini kama kuna mambo hayo watoe ushirikiano. Kama hawawezi kutoa ushirikiano hakuna sababu ya haya mambo kuzungumzwa. Mimi nimecheza mpira, mkiwa mmeshinda kisha anatokea mtu na kuanza kuutia dosari ushindi wenu inauma. Hata mchezaji aliyefunga Hatrick hajisikii vizuri. Wadau watoe ushirikiano, kama hawawezi wakae kimya'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live