Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kama huna tiketi au mwaliko usije uwanjani - TPLB

Kariakoo Dabi Mashabiki Kama huna tiketi au mwaliko usije uwanjani - TPLB

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Bodi ya Ligi (TPLB) Karim Boimanda amesema kama shabiki hajanunua tiketi na hana mualiko asiende uwanjani akitegemea kuingia bure.

Karim amesema kuwa hata vitambulisho vya msimu huu havitatumika katika huo mchezo wa Yanga SC na Simba SC utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

“Kwa wale wageni wanaoalikwa kutazama mchezo huo watapatiwa kadi maalumu ambayo huwezi kumpa mtu mwingine atumie, eneo la VVIP watakaa watu maalumu ambao wamealikwa tu.

“Wengine kama hauna kinachokufanya uingie kiwanjani ni bora usije maana hautaingia uwanjani kwenyewe na watoto tunawapenda lakini siku hiyo wataruhusiwa wale wenye kadi tu,“ alisema Karim.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live