Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kama Yanga tu! Pamba yapiga mtu 5G

Pamba Jiji FC CHAM Pamba Jiji

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuenguliwa nafasi ya pili kwa saa 24, timu ya Pamba FC juzi ilirejea kwenye nafasi hiyo kwa kuifumua Polisi Tanzania mabao 5-1, katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, huku vinara wa ligi hiyo, KenGold wakibanwa mbavu kwa kulazimishwa sare ya 3-3 dhidi ya Mbuni FC.

Kabla ya mechi hiyo, Pamba iliteremshwa hadi nafasi ya tatu, baada ya Mbeya Kwanza kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cosmopolitan na kukwea hadi nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi ya Championship.

Ushindi huo wa mabao 5-1 umeirudisha tena kwenye nafasi ya pili ikifikisha pointi 58, ikibakisha mechi tatu tu za kumalizia msimu na kuisogeza Mbeya Kwanza nafasi ya tatu ikiwa na pointi 56.

Mabao ya washindi yalifungwa na Michael Samamba aliyefunga matatu, lssa Ngoa na Mashaka Adam. Matokeo hayo yanaiweka kwenye nafasi nzuri Pamba kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao moja kwa moja kama itashinda mechi zake tatu zilizobaki.

Wakati hayo yakiendalea, vinara Kengold walishindwa kupata pointi tatu, wakilazimishwa sare ya mabao 3-3 ugenini, Uwanja wa Sheikh Abri Abeid jijini Arusha dhidi ya Mbuni FC.

Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kuendelea kuongoza ligi, lakini ikiwa na pointi 61, sasa ikihitaji pointi tano tu katika michezo mitatu iliyosalia ili kupanda Ligi Kuu.

Iwapo itazipata pointi hizo, itafikisha jumla ya pointi 66, ambazo ni Pamba tu ambayo inaweza kuzipita, huku Mbeya Kwanza kama ikishinda mechi zake tatu zilizobaki, itaishia pointi 65.

Kwingineko tim ya Mbeya City, ikiwa nyumbani, Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ilipata kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya TMA katika mechi ya raundi ya 27 ya ligi hiyo ya Champioship ambayo ipo ukingoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live