Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kally akomalia mastaa Azam FC

Kally Ongala Big Match Kocha wa Azam FC, Kally Ongala

Sat, 20 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Azam kimerejea mazoezini kuendelea na ratiba ya michezo iliyobakia msimu huu huku kocha wa timu hiyo, Kally Ongala akiwataka wachezaji kusahau matokeo yaliyopita ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Namungo.

Akizungumza Kally alisema kuna hali ya kujiamini kupitiliza kwa wachezaji kuona kama msimu kwao umeisha jambo ambalo amewataka kuachana nalo kwa uharaka kwani bado safari ni ndefu.

"Ukiangalia mchezo wetu uliopita kuna wakati wachezaji waliokuwa wanacheza kwa kujiachia sana hivyo kufanya makosa ambayo yalitugharimu ingawa mabao tuliyofungwa ni jitihada za wapinzani wetu," alisema na kuongeza;

"Tuna michezo mitatu ya kumalizia msimu kwa maana miwili ya Ligi na fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hivyo tunahitaji kuhakikisha tunamaliza kwa heshima kisha kuanza hesabu mpya za msimu mwingine ujao."

Michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara kwa Azam ni dhidi ya Coastal Union Mei 24 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga kisha kuhitimisha msimu kwa kupambana na Polisi Tanzania katika mchezo utakaopigwa Mei 28, Azam Complex.

Kipigo cha Azam kutoka kwa Namungo kilikuwa ni cha kwanza kwa timu hiyo kwenye Uwanja wake wa Azam Complex kwani kabla ya hapo mara ya mwisho ilikuwa ni Machi 5, mwaka jana ilipofungwa mabao 2-1 na Polisi Tanzania.

Chanzo: Mwanaspoti