Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kally aita mastaa wake fasta

Kally Ongala Big Match Kocha wa Azam FC, Kally Ongala

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kupoteza ponti mbili dhidi ya Kagera Sugar, kocha msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala ameshtuka na kukaa na vijana wake kuhakikisha makosa hayajirudii kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold leo Jumatano.

Kali ameiongoza Azam FC kwenye michezo tisa, timu yake ikifunga mabao 15 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara nane, akishinda nane na sare moja dhidi ya Kagera Sugar wakifungana mabao 2-2.

Akizungumza Ongala alisema kupoteza kwao pointi mbili ugenini kumeongeza presha ya ushindani na amekaa na vijana wake na kuwaambia kuwa wanatakiwa kusahau matokeo yaliyopita na kuangalia mchezo ulio mbele yao.

“Tuna mchezo mwingine mgumu tumepoteza kwa kuambulia pointi moja tunatakiwa kuwekeza nguvu kwenye mchezo unaofuata ili kuendeleza juhudi zetu za kuhakikisha tunatwaa taji msimu huu kama tulivyopanga,” alisema na kuongeza;

“Hatujakata tamaa tunaendelea kupambana lengo likiwa ni kuhakikisha tunafikia malengo ufikapo mwisho wa msimu, wachezaji wangu wamenielewa na wamerudi kwenye hari ya ushindani natarajia mchezo mzuri dhidi ya Geita Gold Jumatano.”

Ongala alisema wanatarajia mchezo mgumu kutokana na kukutana na timu iliyotoka kujeruhiwa kwa idadi kubwa ya mabao hivyo na wao wanajiandaa kwa ushindani huo ili waweze kupata pointi zitakazowafanya waweze kusonga mbele.

Kally ameiongoza Azam FC kwenye mechi tisa akishinda nane dhidi ya Simba (1-0), Ihefu (1-0), Dodoma Jiji (2-1), Mtibwa Sugar (3-4), Ruvu Shooting (1-0), Namungo (1-0), Coastal Union (3-2), Polisi Tanzania (1-0) na sare moja dhidi ya Kagera Sugar (2-2).

Chanzo: Mwanaspoti