Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalinga: Sikutegema kupata tuzo

Kalina Tuzo Mwamuzi mstaafu wa soka nchini, Elizabeth Kalinga

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mwamuzi mstaafu wa soka nchini, Elizabeth Kalinga amesema tuzo aliyotunukiwa ilikuwa 'sapraizi' kwani hakuwa kuwaza kama anakumbukwa kwenye ulimwengu huu wa sasa tangu astaafu kuchezesha.

Elizabeth ambaye pia ni mwanzilishi wa Shirikisho la Soka la Wanawake Tanzania alitunukiwa tuzo ya heshima kwenye tamasha la Michezo la Wanawake la Tanzanite 2023 lililofanyika wikiendi iliyopita, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti, Elizabeth alisema kuwa; "Sijawahi kupata tuzo yoyote kama hii, ila wakati najishugulisha na soka katika nyanja mbalimbali huko nyuma niliwahi kupata tuzo kadhaa.

"Napenda kuwaambia Wanawake wenzangu walio katika michezo aina zote hata wale watakaokuja baadaye kwamba michezo ni fursa kubwa sana kwetu mtu mmoja mmoja, Halmashauri, Wilaya, Mkoa, Taifa hadi kimataifa.

"Kikubwa wazingatie mazoezi, nidhamu (self displine), umoja na wengine, kujituma, kufuata kanuni na katiba ya mchezo unaoshiriki, ubunifum kutokuwa mbinafsi, uwazi, kuepuka makundi," alisema na kuongeza;

"Ukizingatia hayo utafanikiwa vinginevyo inakuwa sumu mbaya kwako katika maendeleo na mafanikio sehemu yoyote,"

Elizabeth alisema kupewa tuzo hiyo kuonaonyesha namna gani taifa linathamini kazi aliyoifanya wakati wake.

"Tuzo imenifundisha kuwa wema hauozi na cha kale ni Dhahabu, sikuwahi kuwaza kuwa nitakumbukwa, nilijua yakale yamepita, kumbe Mama Samia kaja na muujiza wa tuzo yangu, nimefurahi kupita kiasi.

"Kwa sababu toka 1980/1985 kupata tuzo 21/10/2023 hakika ni muujiza mkubwa, ndani ya miaka 38 sio kitu kidogo kabisa, pia wamebaini kuwa ni mfano mzuri kwa wanawake kuwa kwa kipindi chote hicho tena nikiwa binti," alisema.

Chanzo: Mwanaspoti