Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalidou Koulibaly ajivunia kuipeleka Senegal 16 Bora

Kalidou Koulibaly Kalidou Koulibaly

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa Chelsea, Kalidou Koulibaly ameeleza kujivunia kwake kwa kufunga bao lililoiwezesha timu yake ya Taifa ya Senegal kusonga mbele kwenye hatua ya 16 bora ya Fainali ya Kombe la Dunia.

Koulibaly ameongelea ujumbe wa ”kila la kheri” aliotumiwa na Sadio Mane ambao ulimfanya kupata moto na kufunga bao la kihistoria kwa timu ya Senegal wakati wa mechi yao dhidi ya Ecuador.

”Ilikuwa ni miaka miwili tangu nyota wa nchi yetu Papa Bouba Diop afariki dunia, tulitaka kumfanya ajivunie. Alikuwa hamasa kubwa kwa wachezaji wote.

”Ilikuwa muhimu kuifanya familia yake, familia zetu na Senegal yote , ijivunie. Tulitaka kuonyesha kwanini Senegal ni mabingwa wa Afrika.

”Yawezekana kabisa zaidi ya nusu ya dunia ilidhani hatutopita sababu ya jeraha la Mane. Lakini sisi ni familia, Mane hayupo kwenye mashindano lakini anawasiliana na timu kila wakati, na anachangia kwa kiasi kikubwa kwenye kampeni yetu. Tuna ndoto ya kwenda zaidi ya robo fainali. Tunaendelea kuamini, tunataka kuiandika hadithi ya soka la Senegal.

”Mechi zote ni ngumu, lakini timu itakayofuatia kucheza nasi itaogopa. Wataona tuna talanta, na tunaweza kufanya mambo mazuri,” amesema Koulibaly.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live