Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kali Ongala: Presha inapanda Azam FC

Kali Ongala D.jpeg Kali Ongala

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala, amefunguka kuwa kila mchezo wanaocheza umekuwa mgumu na presha ya hali ya juu katika mzunguko huu wa pili lakini wanapambana ili kumaliza katika nafasi nzuri.

Azam FC ipo nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 47 ikicheza michezo 24 huku ikiwa imebakiza michezo sita kukamilisha mzunguko wa Ligi katika msimu huu wa 2022/23.

Akizungumza na Nipashe jana, Kali alisema mechi za mwisho zina ugumu na presha kubwa, hivyo wanahitaji kupambana ili kuweza kumaliza katika nafasi za juu.

"Tunachotakiwa hivi sasa ni kujiimarisha ili tuwe bora kwa sababu kila mechi inayochezwa inakuwa na presha ya aina yake, ukiangalia huko nyuma tulitoka sare dhidi ya Simba, hivyo tunahitaji kujipanga ili kufanya vizuri katika michezo iliyobaki.

"Muhimu kwetu tunachokiangalia ni alama tatu katika kila mchezo, mfano kwenye mechi ukiongoza goli moja lazima wapinzani wenu na wao watapambana ili warudishe, hivyo tunahitaji kuwa makini, nawasifu wachezaji wangu kwa kupambana," alisema Kali.

Aidha, aliongeza kuwa, anafurahishwa na kiwango cha Prince Dube kutokana na kupambana na kuweza kufunga mbele ya waliomzidi.

"Ninafuraha kuwa na mchezaji aina ya Prince Dube, dogo anajua kupambana kila mechi na kuweza kupata nafasi mbele ya washambuliaji wengine, tunaendelea kumpa mechi tofauti ili aweze kuwa vizuri zaidi," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live