Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalambo arudi Dodoma, bado mmoja

Karibu Dodomaaaa Aaron Kalambo

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Hatimaye aliyekuwa kipa wa Dodoma Jiji, Aaron Kalambo amerudisha majeshi yake kwenye timu hiyo, akifunga idadi ya makipa watatu wa timu hiyo msimu ujao, ambapo amerejea kutokea timu ya Geita Gold.

Kalambo ambaye aliachana na timu hiyo msimu mmoja nyuma, amerudishwa kukamilisha idadi ya makipa kwa Dodoma Jiji ambayo ilikuwa imebaki na makipa wawili, Daniel Mgore na Rakhim Sheik aliyekuwepo msimu uliopita.

Kalambo sasa atakuwa na kazi ya kushindania namba na Mgore kwenye kikosi cha timu hiyo msimu ujao unaoanza Agosti 15, ambapo Dodoma Jiji itacheza mchezo wake Agosti 16 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Wakati Kalambo akirejea, timu hiyo inalazimika kuongeza mshambuliaji mmoja kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mshambuliaji wake Waziri Junior aliyetimkia zake timu ya KMC, kwa makubaliano ya pande zote.

Mshambuliaji ambaye anatajwa kwenye rada za kuziba nafasi hiyo, ni Salum Ngadu ambaye alikuwa kwenye rada za timu ya Fountain Gate inayoshiriki ligi ya Championship.

Wakati wowote mambo yakienda sawa, mshambuliaji huyo aliyeichezea Pamba msimu uliopita, atatangazwa kuwa mchezaji wa mwisho kukamilisha idadi ya wachezji 14 wapya ndani ya timu hiy

Chanzo: Mwanaspoti