Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalaba alikuwa na mke wa rafiki yake kwenye gari iliyopata ajali

Kalaba Ajali Kalaba alikuwa na mke wa rafiki yake kwenye gari iliyopata ajali

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chombo cha Habari cha Lusaka Times, kimeeleza kuwa gari iliyopata ajali ikiwa na nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia na klabu ya TP Mazembe, Rainford Kalaba ilikuwa ikiendeshwa na Charlene Mukandawire mke wa rafiki yake Kalaba aitwaye Boyd Mukandawire.

Mwadada huyo alipoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea Aprili 13, 2024 huko Kafue Zambia huku Kalaba akiwa maututi chini ya Uangalizi wa madakitari Bingwa.

Taarifa zinaeleza kuwa Charlene Mukandawire alimuaga mumewe, Boyd Mukandawire kwamba anaenda kumsalimia rafiki yake huko Kafue kisha baadaye taarifa zikatoka amefariki katika ajali akiwa kwenye Gari ya Rainford Kalaba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live