Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalaba agonga miaka 13 TP Mazembe, atundika daruga

Rainford Kalaba Rainford Kalaba

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuitumikia TP Mazembe kwa takribani miaka 13, winga Rainford Kalaba raia wa Zambia amestaafu soka akiwa na umri wa miaka 36.

Katika kuheshimu mchango wake na utumishi ndani ya TP Mazembe nyota huyo ataendelea kusalia klabuni hapo kama mkurugenzi wa ufundi.

"Baada ya miaka 13 hapa TP Mazembe leo natundika daluga zangu. Shukrani zangu na heshima kuwa sehemu ya familia ya Mazembe kwa wakati wangu niliokuwa hapa kama mchezaji, kamwe sitasahau nyakati mzuri nilipokuwa uwanjani katika jezi ya TP Mazembe pamoja na kuwa nahodha katika maisha yangu ya soka.

“Nina huzuni kuwatangaza kustaafu kwangu kwa mashabiki wangu ulimwenguni kote, haikuwa safari rahisi kwangu, kupongezi kwa juhudi na kujitolea kwangu kwa wakati wote kwenye maisha yangu.

“Nina furaha kuwa nitaendelea kufanya kazi na timu ya ufundi ya TP Mazembe. Hebu tuone safari hii nyingine itatuletea nini. Ahsanteni kwa mara nyingine mashabiki zangu. Mungu awabariki.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live