Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kakolanya atoroka kambini Singida siku ya mechi

Beno Kakolanya Ew Beno Kakolanya

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Goli kipa namba moja wa Singida Fountain Gate Beno David Kakolanya ametoroka kambini ikiwa leo timu yao inacheza mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Yanga SC.

Singida Fountain Gate wametoa taarifa inayosema;

Klabu ya Singida Fountain Gate FC inasikitishwa na kitendo cha mchezaji wetu Beno Kakolanya kutoroka kambini tukiwa tunakabiliwa na mchezo muhimu kabisa dhidi yaYanga leo.

Kitendo hiki kinaleta maswali mengi hasa ukizingatia kuwa Beno na mchezaji

mzoefu na mmoja wa wachezaji wa kutumainiwa wa timu ya Taifa.

Tunaendelea kufuatilia taarifa zake na wachezaji wengine wowote ambao wataonekana kuihujumu timu yetu kwenye mechi ya leo na nyingine zinazofuata.

Mwisho wa kunukuu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live