Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kakolanya atoa neno la shukurani Singida FG

Beno Kakolanya Ew Kakolanya atoa neno la shukurani Singida FG

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda Lango wa Singida Big Stars, Beno Kakolanya ameushukuru uongozi wa timu hiyo kwa kumpa uchezaji bora wa mwezi Septemba wa timu hiyo lakini amesema hayo yasingewezekana bila wachezaji wenzake.

Kakolanya amepewa tuzo hiyo chini ya udhamini wa Kampuni ya Jet & Sons, akiwa ni mchezaji wa kwanza kuchukua tuzo ya mwezi kwa timu hiyo tangu kuanzishwa kwake msimu huu.

“Nimefanikiwa kupata tuzo mwezi Septemba, sijajua kwa miezi inayokuja maana hii ni kutokana na juhudi na mambo mengi uwanjani hasa ushirikiano na wachezaji wenzangu,” amesema Kakolanya.

Kipa huyo ambaye alipewa tuzo hiyo na kitita cha Sh milioni moja, amesema hiyo ni mara ya pili kupata tuzo hiyo kwani aliwahi kuinyakua wakati wa michuano ya Simba Super Cup iliyofanyika mwaka juzi ambapo pia alivuna zawadi ya Sh milioni moja.

Ofisa Habari wa Singida, Hussein Masanza amesema tuzo hiyo ya kwanza imetolewa kwa mujibu wa benchi la ufundi lakini tuzo zinazofuata utaandaliwa mchakato wa wazi wa kuwashirikisha mashabiki kupendekeza mchezaji bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live