Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kakolanya agoma kwenda mbele ya kamati ya maadili

Beno Kakolanya Amechangia Wenzake Kuchapwa Na Yanga   Derick Lissu Beno Kakolanya

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa habari wa Klabu ya Singida Fountain Gate, Hussein Masanza amesema Nahodha na Golikipa wetu, Beno David Kakolanya, amejibu barua ya wito kuwa hatoweza kufika kwenye kikao cha kamati kwa sababu anaamini kamati haitamtendea haki wakati tayari ameshatuhumiwa.

Lengo la wito wa kamati ya nidhamu lilikuwa ni kumpa nafasi ya kujibu tuhuma hizo. Kwa hiyo suala la yeye kukataa wito tunaliacha kwenye maamuzi ya kamati tuone itaamuaje.

Kakolanya alipewa barua ya wito Aprili 15, 2024 ikimtaka kufika mbele ya kamati ya nidhamu Aprili 19 2024 kujibu kuhusu kitendo cha utoro na kuhujumu timu siku chache kuelekea mechi muhimu dhidi ya Yanga SC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live