Golikipa wa Singida Fountain Gate FC, Beno Kakolanya amesema kuwa kipa namba tatu wa Simba SC, Ally Salim kupata nafasi kwenye michezo mikubwa wakati wakiitumika pamoja klabu hiyo ilikuwa ni mpango wa Mungu.
Beno ambaye alikuwa Simba kabla ya kujiunga na Singida amesema kuwa amepata mapokezi makubwa ndani ya Singida BF hivyo ana deni kubwa la kuhakikisha anafanya vyema kuisaidia timu yake hiyo mpya.
Singida FG jana ilicheza mchezo wake wa kirafiki na AS Vita Club ya Vongo na kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika Tamasha la Singida Big Day maalum kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wao wapya.
“Mungu akipanga ucheze unacheza, hata nilipokuwa Tanzania Prisons nilikuwa kipa namba tatu, ilitokea kipa namba moja akaumia, akapewa kipa namba mbili akaharibu ndipo nikapewa mimi, kwa hiyo ikawa mpaka leo mnaniona.
"Naamini ulikuwa muda sahihi ambao Mungu alikuwa ameupanga kwamba Ally Salim adake na ndio muda wake wa kucheza.
“Hakuna kitu ambacho niliharibu, yalikuwa maamuzi ya mwalimu aliona Ally atatusaidia ndiyo maana hata mimi nilikuwa namsapoti," amesema Kakolanya.