Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kakolanya aanika kila kitu kutoroka kambini Singida FG

Beno Kakolanya Ew Kakolanya aanika kila kitu kutoroka kambini Singida FG

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Singida Fountain Gate FC, Beno Kakolanya amefunguka kuhusu taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kuwa ametoroka kambini siku ya mchezo wa Ligi baina ya timu yake na Yanga, saa chache kabla ya kuanza mchezo huo uliopigwa wiki chache zilizopita huko CCM Liti Singida.

Kakolanya ambaye amewahi kupita Mbeya City, Tanzania Prisons, Yanga, Simba kabla ya kutua Singida Fountain Gate amesema kuwa aliomba ruhusa kwa meneja wa timu hiyo siku tatu kabla ya mchezo kutokana na matatizo ya kifalme na akaruhusiwa kuondoka na si kwamba alitoroka kambini kama taarifa ya klabu ilivyoeleza.

“Hivi vitu vipo, wao walitamka vile na wakasema mimi niliondoka siku ya mechi, ukweli ni kwamba mimi sikuondoka siku ya mechi, niliomba ruhusa Alhamisi na nikaondoka siku hiyo usiku, mechi ilikuwa Jumapili. Jiulize, Ijumaa, Jumamosi kwa nini waje waseme siku ya mechi, tena mida ya saa 8 saa 9 ndiyo wanatoa ripoti, huoni kuna kitu hapo.

“Sijawahi kugombana nao na ukiniona ninagombana na timu ujue umeniudhi kwelikweli. Nadhani wao wanajua wana maana gani kusema vile. Mimi niliomba ruhusa na ruhusa ikatoka. Kwenye soka tunaishi na mameneja na mimi niliomba ruhusa kwa meneja, yeye ndiye anakuwa na jukumu la kusema mchezaji flani nimemruhusu ana matatizo haya na haya. Niliondoka nikiwa na ruhusa kwa sababu ya matatizo ya kifamilia.

“Mimi siwezi kususa kwa sababu mpira ndio kazi yangu na familia yangu inapata chakula kupitia huko. Klabu iliniandikia barua niende kwenye Kamati ya Nidhamu, nikamweleza mwanasheria wangu akasema usiende kwa sababu tayari wameshakuhukumu tayari kwenye page yao na vyombo vya habari, kabla ya kukuuliza wewe kwa hiyo hata ukienda huwezi kupata haki yako.

“Hicho kikao ni najisi na kinyume na sheria. Kilichofuata ni kuwajibu kwa barua kuwa sitokuja kwa sababu hii nah ii, kwa hiyo mpaka sasa nasubiri wao watasemaje.

“Kuna vitu sipendi kusema ila inabidi niseme tu. Mtu anaweza kuhoji timu iko kambini kwa nini wewe uko hapa? Mimi niliona tu wameniondoa kwenye, ukiona hivyo unajua kuna kitu kinaendelea, ningekuwa niko kambini lakini baada ya vile mwanasheria wangu akaniambia nenda ukachukue vitu vyako urudi nyumbani kisha tusubiri wataamua nini,” amesema Kakolanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live