Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kakolanya Stars mbona fresh tu

Beno David Kakolanya Kakolanya Stars mbona fresh tu

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Simba, Beno Kakolanya amesema japokuwa anapata nafasi ndogo ya kucheza ndani ya kikosi, lakini kuitwa Taifa Stars kunampa nguvu ya kupambana.

Kalolanya ni mmoja kati ya wachezaji 31 walioitwa Taifa Stars ambayo itaingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Uganda utakaopigwa Machi 24.

Wakati anazungumza Beno alisema inapotokea nafasi ya kucheza humfanya aitumie vyema ili kuonyesha kipaji, jambo linalompa faraja kwani kazi yake inathaminiwa hadi kuonekana Stars.

“Kuna makipa wengi Tanzania, lakini kocha kuona nafaa kuwa miongoni mwa kikosi chake imeniongezea morali ya kazi nikijua ipo siku hadi kwenye kikosi changu nitakuwa chaguo la kwanza,” alisema.

Beno ambaye tangu ajiunge Simba amekuwa namba mbili nyuma ya Aishi Manula aliyeitwa naye Stars, na alisema anapenda ushindani unaomfanya kulinda kiwango chake, akiamini siku akihitajika kwenye majukumu awe tayari kuibeba timu.

“Nimejifunza kujiweka tayari muda wote kwa ajili ya majukumu yangu bila kujali nacheza ama sichezi, kwani najua ilimradi nikiwa kwenye timu kuna siku nitahitaji kufanya kazi,” alisema.

“Nikiwa benchi, nikicheza yapo mengi ninayojifunza kiufundi yanayonifanya niendelee kuboresha kipaji changu, ikifika wakati kila mtu atakiona nachokifanya.”

Ukiachana na Kakolanya, beki wa Kagera Sugar, David Luhende alisema nidhamu ya kazi ndio inafanya aonekane na kuitwa Stars.

“Hakuna njia ya mkato zaidi ya kuheshimu majukumu na kufanya kazi kwa bidii,” alisema.

Wachezaji wengine ambao hawapati nafasi kubwa kwenye vikosi vyao na wameitwa Stars ni kipa Metacha Mnata (Yanga) na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Chanzo: Mwanaspoti