Wakati kikosi cha Singida Fountain Gate kikiwa nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Pili wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Mlinda Mlango wa timu hiyo, Beno Kakolanya ameahidi kufia uwanjani ili kutimiza malengo.
Mwishoni mwa juma hili, Singida itaumana na Future FC ya Misri katika mchezo katika mchezo wa marudiano, baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Azam Complex kumalizika kwa Singida kushinda bao 1-0.
Akizungumza kutoka Cairo, Misri Kakolanya amesema: “Tuliwaona wapinzani wetu kwenye mchezo uliopita, hivyo imani yetu kwa sasa ni kuhakikisha tunaenda kufanya maajabu huko kwao na kwa miujiza ya Mungu naamini unaenda kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.”