Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaka wa Pogba atoka jela kesi ile ya utata

Kaka Pic Kaka wa Pogba atoka jela kesi ile ya utata

Wed, 28 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

KAKA wa Paul Pogba ametolewa jela baada ya kushtakiwa kwa kosa la kumrubuni mdogo wake nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United.

Mathias Pogba alikamatwa Septemba mwaka huu kutokana na tuhuma hizo, lakini sasa ameachiwa huru kwa masharti magumu.

Imeelezwa Mathias amepigwa marufuku kuwasiliana na mdogo wake na ametakiwa kubaki Ufaransa hadi kesi yake itakapomalizika.

Vile vile ndugu huyo wa Pogba amezuiwa kutumia mitandao ya kijamii na endapo atakiuka, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Mathias aliyewahi kuzichezea klabu za Crawley Town, Wrexham na Crewe, aliomba kuachiwa huru tangu Septemba mwaka huu, hata hivyo maombi yake yakapigwa chini na mahakama.

Aidha, Mathias pamoja na watu wengine watano wapo chini ya uangalizi huku uchunguzi ukiendelea na taarifa ziliripoti watu hao walishirikiana na kaka yake Pogba kumrubuni staa huyo anayekipiga Juventus kwa sasa.

Pogba alienda kumshitaki kaka yake kwamba alirubuniwa ili atoe kitita cha Pauni 11 milioni lakini tuhuma hizo zilipingwa vikali na ndugu yake.

Tuhuma hizo ziliibuka baada ya kaka yake Pogba kufichua siri kwamba nyota huyo wa Juventus alikuwa anafanya vitendo vya kishirikina ili amroge Kylian Mbappe, mchezaji mwenzake kwenye timu ya taifa ya Ufaransa.

Pogba alikosa fainali za Kombe la Dunia za Qatar kutokana na majeraha lakini sasa amerejea baada ya kupona na ameanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake huko Turin.

Chanzo: Mwanaspoti