Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaizer wachukua hoteli nzima Dar, ulinzi usipime

Ramada Pic Data Kaizer wachukua hoteli nzima Dar, ulinzi usipime

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

TIMU ya Kaizer Chiefs imeonyesha kuwa wapo makini na mchezo wa marudiano dhidi ya Simba baada ya kuamua kuchukua hoteli pembeni ya mjini huku wakiweka ulinzi mkali.

Timu hiyo kutoka Afrika Kusini iliwasili jana Mei 20, 2021 na moja kwa moja walienda katika hoteli ya Ramada iliyopo Mbezi Beach.

Mwanaspoti lilipopita katika hoteli hiyo lilisimama na kushuhudia ulinzi uliopo huku mtu anayeingia wanatoka watu wa Kaizer na kuzungumza nae kisha unageuka na kuondoka.

Inaelezwa mabosi wa Kaizer Chiefs wameichukua hoteli hiyo nzima mpaka watakapoondoka kesho baada ya mechi yao dhidi ya Simba.

Mazingira katika hoteli hiyo kulikuwa ni utulivu wa hali ya juu huku kukiwa na magari machache tofauti na ilivyozoeleka kuwa na magari mengi yakiwa yamepaki nje na ndani ya hoteli hiyo.

Pia Kaizer inaelezwa jana baada ya kuwasili walikataa gari lilioandaliwa na Simba kisha wakaingia katika gari waliloandaa wao kutoka kampuni ya Shabiby. Awali timu ziizocheza na Simba zilikuwa zinafikia HoteliĀ  ziiizopo mjini, lakini imekuwa tofauti kwa Kaizer Chiefs ambao wapo mbali na uwanja wa mchezo (Benjamin Mkapa).

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz