Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaizer Chiefs yarudi kwa Nabi

Nabi Molefi Ntseki Kaizer Chiefs yarudi kwa Nabi

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imefufua tena mbio za kuwania saini ya kocha wa FAR Rabat, Nasreddine Nabi.

Chiefs maarufu kwa jina la Amakhosi hii ni mara ya pili kuhitaji huduma ya Nabi ambapo awali wakati kocha huyo akiachana na Yanga walikaribia kunasa saini yake kabla ya kocha huyo kubadili akili yake na kutua Rabat.

Amakhosi baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wao Molefi Ntseki waliyeanza naye msimu huu walimchukua Cavin Johnson ambaye alikuwa mkuu wa maendeleo ya soka la vijana kukiomgoza kikosi hicho.

Mabosi wa Amakhosi bado wanaona chaguo sahihi kwao ni Nabi kuja kurudisha utulivu wa timu hiyo inayoshika nafasi ya 7 kwenye ligi ya nchini humo ikicheza mechi 11 ikikusanya alama 14.

Nabi ameendelea kuwa na wakati mzuri Rabat akiifanya kuongoza msimamo wa ligi wakikusanya alama 17 baada ya kucheza mechi 8.

Uongozi wa Amakhosi wamekuwa kwenye presha kubwa ya mashabiki wao wakiona wameshindwa kuirudishia makali timu hiyo wakichukizwa na hatua ya vinara wa ligi Mamelodi Sundown kuendelea kuwa wababe kwa miaka kadhaa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live