Vyombo vya Habari nchini Afrika Kusini, vimeripoti kuwa, Klabu ya Kaizer Chiefs haina mpango wa kumsajiri mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele bali Klabu ya Mamelodi Sundowns ndiyo inamhitaji mshambuliaji huyo.
Taarifa zinaeleza kuwa kipindi timu ipo Afrika Kusini, Rais Wa Klabu Wa Yanga walikutana na kujadili ili kukamilisha dili hilo na rais klabu ya Yanga awaliwambia wasubiri ligi imalizike ili waweze kukamilisha usajiri huo.
Mara kadhaa Yanga imekuwa ikisisitiza kuwa haina mpango wa kuwauza wachezaji wake muhimu wakiwemo Fiston Mayele ambaye amekuwa na manufaa makubwa kwa klabu hiyo katika Ligi ya ndani na Kimataifa.
Mayele ndiye kinara wa mabao Ligi Kuu Bara mpaka sasa akiwa na mabao 16 huku pia akiongoza kwa mabao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na mabao 6 sawa na Ranga Chivaviro wa Marumo Gallants.
Aidha, mwishoni mwa msimu uliopita, pamoja na virabu vingine vya Kaskazini mwa Afrika, Kaizer nao walionyesha nia ya kumtaka Mayele lakini klabu yake iligoma kumuuza na badala yake aliongezewa mkataba mpaka mwaka 2024.