Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kai Havertz ndani ya viunga vya Emirates

Kai Havertz Goal Kai Havertz

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Asilimia 65% za mashabiki wa Arsenal walimpigia kura Kai Havert kuwa mchezaji bora wa mwezi November ndani ya kikosi hicho mbele ya Willo Saliba, Bukayo Saka na Leandro Trossard kama Standout Perfomer.

Jamaa alianza kukiwasha pale Ujerumani baada ya Julian Nagelsmans kumuweka Left-back na kufunga bao, baada ya hapo akarejea klabuni na Arteta akaendelea kumuamini.

Kwenye game dhidi ya BRENTFORD akafunga bao lake la pili ndani ya kikosi hicho dakika ya 89 ya mchezo na kuipa Arsenal ushindi.

Baada ya hapo akafunga kwenye Uefa game dhidi ya Lens kwenye ushindi wa mabao (6-0) wakiwa Emarates kabla ya kufunga tena akiisawazishia Gunners bao la pili dhidi ya Luton kabla ya Rice kuweka chuma cha ushindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live