Kiungo wa kati wa Arsenal Kai Havertz ameandika chapisho la kihisia siku ya Jumatatu kufuatia kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza wa 2023/24 siku ya Jumapili.
Msimu wa EPL 2023/24 ulimalizika jioni ya Mei 19, wakati Mabingwa watetezi Mancehester City walipotwaa taji hilo kwa mara ya nne mfululizo. Vijana wa Pep Guardiola walishinda klabu ya West Ham United 3-1 kwenye Uwanja wa Etihad na kujihakikishia kombe la mwaka huu wakiwa na pointi 91, huku Arsenal wakimaliza nafasi ya pili wakiwa na pointi 89 baada ya kuifunga Everton 2-1 kwenye uwanja wa Emirates.
Katika chapisho lake la siku a Jumatatu, Havertz alizungumzia jinsi klabu yake mpya imemsaidia kukuza taaluma yake ya soka katika mwaka mmoja uliopita.
Pia alitoa shukurani zake kwa mashabiki wa Arsenal, wakufunzi na wachezaji wenzake kwa sapoti waliyomuonyesha katika msimu uliomalizika