Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kahraba, Percy Tau wamvuruga Kocha Al Ahly

Al Ahly Percy Tau Kahraba, Percy Tau wamvuruga Kocha Al Ahly

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marcel Koller; Kocha Mkuu wa Al Ahly ameendelea kulia na safu yake ya ushambuliaji kuwa ni butu msimu huuu.

Al Ahly walishindwa kupata bao mbele ya CR Belouizdad licha ya kukamata mchezo Kwa muda mrefu na walitengeneza nafasi nyingi ambazo walishindwa kugeuza zikawa mabao.

Percy Tau, El Shahat na Kahraba wameshindwa kuwa tishio Kwa walinzi wa timu pinzani msimu huu katika michuano mbali mbali wanayoshiriki Al Ahly ambapo hawajapa ushindi katika michezo mitatu ya mwisho (wametoa sare yote).

Ndani ya dakika 270 Al Ahly wamefunga bao moja tu katika michuano yote yaani mechi tatu wamepata bao moja ambalo walifunga kwa Mkapa dhidi ya Yanga SC licha ya kutengeneza nafasi zaidi ya 15 ambazo wangekuwa na utulivu wangefunga mabao.

Koller amesema Washambuliaji wake lazima waje upya katika mchezo wa marudiano huko Algeria ???????? dhidi ya CR Belouizdad kama wanataka kufanya vema ndani ya CAF Champions League msimu huu.

Kumbuka ushindi wa Ahly dhidi ya CR Belouizdad utakuwa na faida kubwa sana kwa timu ya Wananchi Yanga kama nayo itavuna alama tatu dhidi ya Mediama.

Al Ahly, Mamelodi Sundowns na Wydad Athletic Club wamecheza mechi 13 ndani ya siku 66, ambapo ndani ya siku hizi unatoa muda wa mapumziko ya kalenda ya FIFA.

Al Ahly mechi -13 miezi miwili

Wydad Athletic mechi -13 miezi miwili

Mamelodi Sundowns mechi -13 miezi miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live