Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagoma aikana Yanga, akomaa na Simba

Kagoma Simba Mz Yusuph Kagoma

Sun, 11 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) leo ikikaa jijini Dar es Salaam kujadili shauri la kiungo Yusuf Kagoma, upande wa mchezaji huyo umesema kuwa unatambua anastahili kuchezea Simba.

Kagoma amewekewa pingamizi na Yanga inayodai ni mchezaji wake ikisema kuwa alisaini mkataba wa kuitumikia kabla ya kuamua kusaini mkataba mwingine wa Simba ambayo yupo nayo hivi sasa.

Wakili wa Yusuf Kagoma, Leonard Richard amesema mchezaji huyo ni mali halali ya Simba kwa mujibu wa makubaliano na usajili alioufanya na timu hiyo.

"Tumeiomba kamati itupe muda ili tuweze kupitia yale yaliyowasilishwa na Yanga tunashukuru kamati imeridhia maombi yetu na tumeambiwa haitachukua muda hadi Agosti 20 kikao kitafanyika.

"Kuhusiana na Kagoma kusaini mkataba timu zote mbili hili naamini wao watu sahihi watakaotoa taarifa juu ya mkataba sahihi uliosainiwa na karatasi ya makubaliano ya awali.

"Mimi ninachokifahamu Kagoma ni mchezaji halali wa Simba sio kila karatasi linalosainiwa ni mkataba hili naomba nisilizungumze sana watu sahihi ni viongozi wa kamati ambayo tuna imani nayo itatoa majibu sahihi," alisema Richard.

Akizungumzia suala la mchezaji huyo kutokucheza tangu amejiunga na timu hiyo alisema haihusiani kabisa na masuala ya kimkataba changamoto ni kiungo huyo kutokuwa timamu kama walivyo wachezaji wanaocheza eneo lake.

"Kagoma hayupo fiti eneo analocheza waliopo wapo tayari japo sitakiwi kulizungumzia hili sana kocha ndio anatakiwa kutoa huu ufafanuzi ila uhakika ni kwamba haihusiani na suala la kimkataba kwasabu ni mali halali ya Simba," alisema wakili huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live