Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere kuwakabili waajiri wake wa zamani

Kagere Meddie Ee Meddie Kagere

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa zamani wa Simba Meddie Kagere ataongoza safu ya ushambuliaji ya Singida Big Star dhidi ya waajiri wake hao.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Leo katika dimba la Liti saa 10 jioni.

Kocha wa SBS Hans Van Pluijm amewanzisha pamoja Kagere na Rodrigo Tegu.

Golini ataanza kipa wa zamani wa Geita Gold,Khomeny Abubakary.

Abukabakry amepata nafasi hiyo mara baada ya Benjamini Haule kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania.

Beki wa kulia Pluijm amemwanzisha Paul Godfrey huku kushoto akicheza nahodha Shafiq Batambuzi.

Mabeki wa kati wameanza Abdul Majid Mangalo na Biermes Carno huku namba sita akicheza Bruno Gomes

Winga ya kulia ameanza Deus Kaseke na kushoto ni Dario Fiedrico na dimba kubwa akianza Said Ndemla.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na timu zote kupata ushindi katika michezo uliyopita.

SBS waliwafunga Polisi Tanzania bao 1-0 huku Simba wakiwafunga Mtibwa Sugar 5-0.

Timu hizo zina pointi 17 zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa ambapo Simba inashika nafasi ya 2 huku Singida ikishika nafasi ya nne

Chanzo: www.tanzaniaweb.live