Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere awasha moto Simba SC yaichakaza Singida United kwa mabao 8-0

98719 Pic+simba Kagere awasha moto Simba SC yaichakaza Singida United kwa mabao 8-0

Thu, 12 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya kupoteza katika mchezo uliopita dhidi ya watani zao Yanga, Simba leo imeishusha kipigo kizito dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru. Huku kikosi chao cha kwanza kikionekana kuwa na mabadiliko ya wachezaji kadhaa Simba wameibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Singida United inayoburuza mkia katika msimamo wa Ligi hiyo. Meddie Kagere ambaye alicheza John Bocco katika safu ya ushambuliaji ya Simba ndiye aliyeibuka shujaa katika mchezo huo kutokana na kufunga mabao manne katika dakika ya 2, 26, 41 na 71. Mabeki wa Singida United, wakiongozwa na Tumba Swedi 'Mdudu Kiwi' ambaye aliwahi kutamba akiwa Stand United, walishindwa kumdhibiti mshambuliaji huyo hatari. Mabao manne ya Kagere katika mchezo huo, yamemfanya kuendelea kujitengenezea mazingira akiwa na mabao 19 ya kubeba kiatu cha mfungaji bora kwa msimu wa pili mfululizo. Mbali na Kagere mabao mengine ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na Deo Kanda ambaye alitupia mawili, Bocco na Sharaf Shiboub waliofunga bao moja kila mmoja. Ndani ya dakika zote za mchezo Simba walionekana kumiliki mpira kwa asilimia kubwa huku kocha wa kikosi hicho akionekana kufanya mabadiliko kadhaa kwa lengo la kuwapumzisha wachezaji wake baada ya kuwa na uongozi wa mabao mengi, akiwemo Shomary Kapombe. Katika mchezo huo, Singida United iliwalazimu kumaliza wakiwa pungufu baada ya kiungo wao, Haruna Moshi 'Boban' kuonyesha kadi nyekundu baada ya kuchezea vibaya, Aishi Manula. Kikosi cha Simba, Aishi Manila, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Tairone Santos, Pascal Wawa,Jonas Mkude, Deo Kanda, Luis Miquissone, Meddie Kagere, John Bocco na Hassan Dilunga. Kikosi cha Singida United, Owen Chaima, George Wawa, Haji Mwinyi, Meshack Kibona, Tumba Swedi, Cleophace Sospeter, George Sangija, Haruna Moshi 'Boban', Steven Sey, Seiri Arigumaho na Mtikila Hussein.

Chanzo: mwananchi.co.tz