Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere atupia Simba SC ikiichapa Namungo

93694 Pic+simba Kagere atupia Simba SC ikiichapa Namungo

Thu, 30 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji Meddie Kagere amefunga bao dakika 87, Simba ikichapa Namungo kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mshambuliaji Kagere alifunga bao hilo akiwa katika eneo la kuotea, alipokea pasi ya John Bocco na kumchambua kipa wa Namungo. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na viungo Francis Kahata na Hassan Dilunga wakati yale ya Namungo yalipachikwa wavuni na Bigirimana Blaise na Lucas Kikoti. Ushindi huo unaifanya Simba kupata kileleni ikiwa na pointi 43, na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake msimu huu. Namungo walikuwa wanacheza mpira wa utulivu na pasi za haraka haraka huku wakiwatumia viungo wao, Daniel Jolam na Lucas Kikoti kuhakikisha wanaisogeza timu yao mbele. Katika eneo la kiungo Simba kulikuwa na Jonas Mkude, Sharaf Shiboub na Ibrahim Ajib ambao nao walionekana kuwa fiti na kufanya eneo hilo kuchezeka mchezo wa kuvutia. Dakika 21 Simba ilipata goli la kwanza baada ya Shomari Kapombe kupiga krosi na Francis Kahata alionganisha mpira huo kwa kichwa na kwenda moja kwa moja wavuni. Baada ya goli hilo Namungo walionekana kutokata tamaa na dakika 35, Blaise aliisawazishia baada ya Kikoti kupiga krosi iliyomkuta Mrundi huyo akiwa peke yake baada ya mabeki wa Simba, Pascal Wawa na Erasto Nyoni kujichanganya. Simba iliwachukua dakika 3 tu (dakika 38) kuongeza goli baada ya Hassan Dilunga kukunjuka shuti kali nje ya 18 na moja kwa moja kwenda wavuni. Mabeki wa Namungo, Stephen Duah na Kalos Protus walijitaidi kumzuia mshambuliaji wa Simba, Kagere ambaye alionekana kuhaha kupenya ngome hiyo. Dakika 56 Simba walifanya mabadiliko ya kumtoa Ibahim Ajib na kuingia Clatous Chama huku Namungo wakimtoa George Makanga na kuingia Hamis Halifa. Simba walianza kutumia mbinu za kupiga mashuti ya mbali na dakika 57, Hassan Dilunga alipiga shuti nje ya 18 na kuwa kona isiyokuwa na faida. Dakika 70 Namungo walisawazisha kupitia kwa kiungo wao Lucas Kikoti baada ya kufyatuka shuti kali nje ya boksi na kwenda moja kwa moja wavuni. Simba ilifanya mabadiliko dakika 71 kwa kumtoa Hassan Dilunga na kuingia John Bocco huku beki wa Namungo, Kalos Protas akipewa kadi ya njano baada ya kuonekana kuzozana na muamuzi wa kati, Florentina Zabron. Mpira uligeuka kuwa na ufundi mwingi, mabavu na kasi kwa kila timu huku kila mmoja akionyesha kutaka kupata goli Namungo walitaka kupata goli dakika 83 baada ya Lucas Kikoti kupiga pasi mpenyezo kwa Abid Athuman na wakati akijipanga kupiga shuti kipa wa Simba, Beno Kakolanya alitokea na kuucheza mpura huo. Mchezo ulikuwa wa piga nikupige na dakika 84, kiungo Clatous Chama alitaka kufunga goli la ushindi baada ya kuwatoka mabeki na kufyatuka shuti lakini liliishia mikononi mwa Abarola. Dakika 87 Meddie Kagere aliwainua mashabiki wa Simba baada ya Bocco kuuchopu mpira na Shiboub kuupiga mpira huo kwa kichwa na kutua miguuni kwa Kagere aliyepiga shuti la pembeni na kwenda moja kwa moja wavuni.

Chanzo: mwananchi.co.tz