Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere atoa ufafanuzi ushangiliaji wake

Kagere Unafiki Kagere atoa ufafanuzi ushangiliaji wake

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Mshambuliaji kutoka nchini Rwanda na Klabu ya Singida Fountain Gate, Meddie Kagere amesema kuwa ujumbe wake aliouandika kwenye fulana baada ya kufunga kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ni aina ya ushangiliaji aliochagua.

Juzi Jumatatu (Novemba 27) Kagere alifunga bao lake la kwanza kwenye ligi msimu huu 2023/24, na wakati wa kushangilia alionyesha fulana iliyoandikwa “Mnafiki ishi naye kinafiki” katika mchezo ambao uliisha kwa Singida kushinda mabao 2-1.

Kagere amesema kuwa: “Maisha ya duniani tunaishi kinafiki lakini sisi wote tukiishi kwa umoja bila kuonyesha unafiki kwa umoja itakuwa vizuri.

“Tunaishi na watu ambao wanacheka lakini hawana ushirikiano. Ni ujumbe wangu ambao unakwenda na kazi ambayo ninafanya na namna ya ushangiliaji lakini ninamshukuru Mungu.”

Chanzo: Dar24