Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere, Wawa, Banda wavunjiwa mikataba Simba

Meddie Kagere Kagere, Wawa, Banda wavunjiwa mikataba Simba

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KLABU ya soka ya Simba imevunja mikataba ya nyota wake wanne wa kigeni wakiwemo mastaa wao aliokuwa tegemeo katika kikosi hicho kwa misimu kadhaa, beki wake Raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa na mshambuliaji wake, Mnyarwanda, Meddie Kagere.

Mbali na mastaa hao wawili tegemeo, nyota wengine wa kimataifa waliotemwa ni Peter Banda aliyesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili mwezi Agosti na kiungo mshambuliaji Dancan Nyoni Raia wa Malawi ambaye ameshindwa kuonesha makali yake toka asajiliwe klabuni hapo.

Simba imeamua kuvunja mkataba na wachezaji hao, ili kupata nafasi ya kusajili wachezaji wengine wa kigeni kwenye dirisha dogo la usajili.

Pascal Wawa Ikumbukwe hivi karibuni klabu hiyo ilivunja mkataba kwa makubaliano maalumu na kocha wake msaidizi Thiery Hitimana raia wa Burundi.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameamua kufanya maboresho kwenye kikosi chao kufuatia kusuasua hivi karibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live